Kuvua soksi na kuosha miguu ni kukhalifu Sunnah


Swali: Wakati ninapotawadha kwa ajili ya swalah wakati mwingine nakuwa mwenye kuvaa soksi za kawaida na hufuta kwa mkono wangu juu ya soksi kwa maji pamoja na kuzingatia kwamba soksi hizo ni safi. Je, inafaa kufanya hivo?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah kwa muislamu ni yeye kufuta juu ya soksi za kawaida au soksi za ngozi akizivaa akiwa na twahara na huku amefunika miguu na vifundo. Mchana mmoja na usiku wake kwa ambaye ni mkazi na michana mitatu na nyusiku zake akiwa ni msafiri. Muda unaanza kuhesabiwa kuanzia mpanguso wa kwanza baada ya kupatwa na hadathi. Akizivua na akaosha miguu baada ya kuosha uso, mikono, kufuta kichwa na masikio hakuna neno. Lakini hivyo ni kwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/107)
  • Imechapishwa: 14/08/2021