Kuvua mavazi aliyozowea kuvaa mtu anaposafiri miji ya makafiri

Swali: Ni ipi hukumu kwa mtu anapoenda katika mji wa kikafiri anavaa mavazi yao na havai mavazi wanayovaa watu wa mji wake. Je, mtu huyu anazingatiwa kuwa ni mwenye kujifananisha [na hao makafiri]?

Jibu: Ndio, anazingatiwa kuwa ni mwenye kujifananisha. Isipokuwa ikiwa kama ataendelea kuvaa mavazi yake anakhofia juu ya nafsi yake na mali yake. Hili likamfanya kuvaa mavazi yao ili kuepuka shari yao. Katika hali hii ameruhusiwa. Ama akiwa anavaa kwa ajili ya mapenzi na wala haogopi, bali kilichomfanya kufanya hivo ni kwa sababu ya kutaka kujifananisha nao haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2122
  • Imechapishwa: 02/07/2020