Kuvaa nguo yenye manii


Swali: Je, inafaa kuvaa nguo ilio na manii kidogo?

Jibu: Manii ni masafi/twahara. Lakini yanaondoshwa kwa ajili ya usafi. Vinginevyo ni masafi. Yanaondoshwa kama ambavo ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa akiyaondosha kutoka kwenye nguo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha anaisafisha. Anafanya hivi kwa minajili ya usafi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 16/09/2018