Kuvaa kiatu kimoja wakati wa kukaa

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa kiatu kimoja? Ikiwa mtu amekaa juu ya kiti na hatembei kitendo hicho kinaingia pia ndani ya makatazo?

Jibu: Kumepokelewa makatazo ya kuvaa kiatu kimoja. Udhahiri wa hilo ni pale mtu anapotembea. Akiwa mtu amekaa ni jambo halizingatiwi.

Jambo hili sahali. Haidhuru ikiwa atakivaa wakati mfupi. Lakini hata hivyo haitakiwi kwa mtu kuvaa kiatu kimoja kwa muda mrefu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 02/03/2019