Kuuza vitabu vya kielimu katika masoko ya Bid´ah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuanzisha masoko ambayo kunauzikana vitabu vya kielimu pamoja na kuzingatia kwamba katika masoko haya kunaweza kufanywa Bid´ah kwa mfano Bid´ah ya Maulidi na Bid´ah nyenginezo? Je, kuuza vitabu vya kielimu kunahesabika ni kuwasaidia katika Bid´ah?

Jibu: Hapa kuna mambo mawili:

La kwanza: Bid´ah ni kitu kimoja. Asishirikiane nao katika Bid´ah.

La pili: Kuuza vitabu ni kitu kingine. Isipokuwa ikiwa kama kuuza kwake anawashaji´isha katika Bid´ah. Katika hali hii asiuze katika wakati huu. Atenge muda mwingine wa kuviuza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 02/03/2019