Kuuza chakula na tamtam kwa ajili ya maulidi

Swali: Inajuzu kuuza chakula na vitu tamtam vinavyofanywa katika usiku wa mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Haijuzu kwa watu kuanza kufanya kupatikane vitu katika misimu ambayo hakukupokelewa chochote katika Shari´ah. Hawana haki ya kufanya hivo wala kukhusisha kwa kitu. Mambo yote yanatakiwa kujengeke juu ya dalili na juu ya Sunnah. Ama watu kutegeza msimu huo wa sikukuu na minasaba ambayo watu wanaisherehekea ambapo wakafanya chakula aina mbalimbali ni kitendo kiovu. Haifai kwa mtu kukhusisha siku ambayo haikushusishwa na Shari´ah kwa sifa yoyote ya kipekee; si kwa kuandaa chakula, kutoa swadaqah na wema katika mnasaba huo maalum.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 08/11/2019