Kuunganisha nywele haijuzu


Swali: Ni ipi hukumu ya kuunganisha nywele za wanawake?

Jibu: Kuunganisha nywele haijuzu. Hapana tofauti kati ya nywele za wanadamu na za viumbe wengine ambavyo nywele zao zinaweza kuunganisha. Hayo ni kutokana na kuenea kwa Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa zinazokataza juu ya jambo hilo. Katika “as-Swahiyh” ya Muslim kutoka kwa Asmaa´ bint Abi Bakr (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia: “Kuna mwanamke mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Msichana wangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake. Je, niziunganishe?” Akamjibu: (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Allaah amemlaani mwenye kuunganisha nywele na mwenye kuungwa.”

Imepokelewa pia kutoka kwa Abu az-Zubayr kwamba amemsikia Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) akisema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amegombeza mwanamke kuunganisha chochote kwenye nywele zake.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/52)
  • Imechapishwa: 07/08/2021