Swali: Je, kufanya chuku ni miongoni mwa mambo yanayochengua wudhuu´? Je, ni miongoni mwa mambo yanayoharibu swawm ya sunnah?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana katika jambo hili. Hakuna dalili ya wazi inayoonyesha kuwa damu nyingi inaharibu swawm. Lakini hata hivyo wanachuoni wengi wanaona kuwa damu nyingi inachengua wudhuu´. Hivyo mtu atawadhe kwa ajili ya usalama zaidi. Kwa ajili hii al-Bukhaariy ameweka mlango unaosema: “Mlango wale wasioonelea kutawadha isipokuwa tu kwa chenye kutoka kupitia tupu ya mbele na ya nyuma”. Amesema kwamba kuhusu kwamba damu inachengua wudhuu´ kumapokelewa Hadiyth ilio na udhaifu. Lakini ikiwa damu nyingi wanachuoni wengi wakiwemo Hanaabilah wanaona kuwa ni miongoni mwa mambo yanayochengua wudhuu´.

Vivyo hivyo kuumikwa kwa yule ambaye amefunga. Maoni ya sawa ni kwamba kufanya chuku kunaiharibu swawm. Ni mamoja funga hiyo ni ya faradhi au iliyopendekezwa. Wanachuoni wengi wanaona kwamba swawm haiharibiki na kwamba hukumu hiyo imefutwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 25/05/2019