Kutumia Ruqyah na dawa


Swali: Je, inatosha kuchukua Ruqyah peke yake bila ya kuchukua dawa ili maradhi yapone bila kujali maradhi yoyote yale? Kujisomea mwenyewe Ruqyah au kuomba mtu amsomee kunamtoa katika wale watu 70.000 watakaoingia Peponi bila ya hesabu wala adhabu?

Jibu: Muislamu asitosheke kwa kutumia Ruqyah peke yake, bali atumie Ruqyah na dawa zinazoruhusiwa. Yote yanatoka kwa Allaah na ni kheri. Atumie hili na hili. Atumie dawa zinazonufaisha na awaombe ushauri matatibu wenye fani hiyo. Hali kadhalika atatumia Ruqyah. Kwa kuwa huku ni kufanya sababu, na asiishie kufanya sababu moja tu. Hili halina makatazo yoyote, ya kuwa akakusanya baina ya Ruqyah na kutumia dawa zinazoruhusiwa. Na zote ni sababu zenye kheri na kunatarajiwa manufaa (dawa) kwa idhini ya Allaah. Hakuna kuzuizi kinachomzuia mtu kuwa katika wale watu 70.000 akijisomea Ruqyah mwenyewe. Ni yule ambaye anaomba wengine wamsomee Ruqyah, huyu ndiye yule ambaye haingii kwa wale watu 70.000. Lililotajwa katika Hadiyth ni kuwa hawaombi wengine wawasomee Ruqyah, haina maana kuwa hawatumii Ruqyah kabisa. Maana yake ni kuwa, hawaombi wengine wawasomee Ruqyah. Kwa nini? Kwa kuwa wakiomba wengine wawasomee Ruqyah watakuwa wamewaomba watu. Kinachotakiwa ni kutowaomba watu, badala yake mtu mwenyewe ndio ajisomee Ruqyah na wala asiwahitajie watu. Mtume (´alayhis-Salaam) anasema, miongoni mwa sifa zao ni kwambahawawaombi watu wengine wawasomee Ruqyah kwa kujitosheleza kwao kwa Allaah (Ta´ala) Pekee.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=hSdHjgz2sPg
  • Imechapishwa: 23/03/2018