Swali: Leo kunaongelewa sana kuhusu mada ya Ruqyah. Baadhi ya watu wanachukulia sahali na wengine wanakazia. Baadhi ya watu wanafanya Ruqyah kwa yanayoafikiana na Sunnah na wengine wanafanya kwa Ijtihaad zao. Na ipi nasaha yako kwa wale wanaojishughulisha na Ruqyah?

Jibu: Leo Ruqyah inafanywa kwa kutafuta pesa. Wamejiingiza katika hili wasiyoistahiki. Wanafanya hivyo kwa kutafuta pesa. Hali kadhalika, wamejishughulisha nayo watu ambao ´Aqiydah zao ni mbovu kwa kutafuta pesa. Na kuna watu wamejiingiza kwayo wanaichanganya (Ruqyah hiyo) na mambo ya kishirki na hirizi. Yote haya yanafanywa kwa ajili ya kutafuta pesa. Leo Ruqyah imekuwa ni riziki na biashara. Na hili ni jambo halijuzu. Haijuzu isipokuwa kwa mtu ambaye ni mjuzi wa Ruqyah, mwenye ´Aqiydah nzuri na anataka kihakika kumnufaisha ndugu yake na si kwamba anachotaka yeye ni pesa tu. Lengo lake ni kutaka kumnufaisha ndugu yake mgonjwa. Na ikitokea akapewa kitu katika mali, haina neno akakichukua.

Ama kuichukulia kuwa ndio riziki kwa kufungua maduka, huku ni kuchupa mipaka kwa Ruqyah na ni jambo linalofanywa kwa kutaka (kulenga) pesa tu na si kutaka kuwanufaisha watu, Kunaweza kupenyeza ndani yake – kama tulivyosema – wanganga na wachawi na wakasoma katika vitabu vya kiganga, wakawasomea watu ili wachume pesa. Kwa kuwa kuna vitabu vya kiganga kwa [kutumia] jina la Ruqyah. Ndani yavyo kuna uchawi, shari, kutafuta kinga kwa majini na Mashaytwaan, kuna utafutaji msaada kwa asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jalla). Ni lazima mwenye kufanya Ruqyah awe ni mtu mwenye elimu, Baswiyrah, kuaminika na awe na ´Aqiydah nzuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=cHdTE5Brz3c
  • Imechapishwa: 23/03/2018