Kutumia manukato yaliyo na alcohol


Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia uturi na manukato ambayo yamo ndani alcohol?

Jibu: Kimsingi ni kwamba ni uhalali uturi na manukato yaliyo kati ya watu. Isipokuwa yale ambayo yana kizuizi cha kuyatumia kwa sababu yanalevya, mengi yake yanalevya, ndani yake mna najisi na mfano wa hayo. Vinginevyo kimsingi ni uhalali wa uturi aina mbalimbali ulioko kati ya watu.

Ikiwa mtu atajua kwamba kuna uturi ambao una kizuizi cha kuyatumia katika kilevi au najisi basi anatakiwa kuyaacha. Miongoni mwa hayo ni cologne ambayo imetuthibitikia kwa ushahidi wa madaktari kwamba hayakusalimika na ulevi. Ndani yake mna kiasi kikubwa cha esperto, nao ni ulevi. Kwa hivyo ni lazima kuiacha. Isipokuwa kukipatikana aina iliosalimika na miongoni mwa manukato mengine aliyohalalisha Allaah. Vivyo hivyo ni lazima kuepuka kila kinywaji na chakula kilicho na kilevi. Kanuni inasema:

“Kingi kinacholevya basi kingi chake pia ni haramu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kingi kinacholevya basi kingi chake pia ni haramu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/41)
  • Imechapishwa: 29/08/2021