Kutumia dawa ya kuzuia mimba kutokana na uzito anaoupata mwanamke

Swali: Kuna mwanamke ana mtoto mdogo ambaye ana miezi kumi na kwa sasa ana ujauzito mwingine. Anahisi uzito wa kutazama watoto wake na ubebaji wa mimba. Je, baada ya mimba hii mpya naweza kutumia dawa ya kuzuia mimba?

Jibu: Tunachomnasihi, amkabidhi amri yake Allaah. Na akikhofia juu ya nafsi yake maangamivu na akaambiwa na matabibu wenye fani hii huenda akafikwa na maangamivu na akafa, hapo anaweza kutumia dawa hiyo. Tunachomnasihi ni yeye amtegemee Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na amkabidhi amri yake Allaah (´Azza wa Jalla).

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3068
  • Imechapishwa: 01/03/2018