Kutukana familia ya kifalme ya kisaudi ni fitina ya upofu

Nafikiri kwamba ambaye anataja upokezi huu[1] yuko pamoja na ile fitina ya ´Iraaq dhidi ya Kuwait na miji mingine yote ya kiarabu dhidi ya Saudi Arabia. Wao wanataka kutendea kazi Hadiyth hii juu ya mtawala wa Saudi Arabia. Watu hawa walikuwa wapi kabla juu ya msimamo wa upokezi huu au Hadiyth hii isiyokuwa na uwepo?

Najua tangu miezi mingi ya nyuma kwamba kuna waandishi wa kisiasa ambao wameandika kitabu dhidi ya wafalme wa kisaudi akiwemo mfalme aliyeko hivi sasa. Wakataka kukichapisha katika baadhi ya maduka ya uchapishaji nchini humu, lakini yakakataa kwa kuchelea kusababisha matatizo ya kisiasa. Kwa masikitiko fitina hii ya upofu imezuka. Badala yake wakaanza kueneza karatasi ndogondogo. Mimi sijafikia na chochote katika hayo. Ndani yake kuna Hadiyth ikiwa ni pamoja na hii ambayo si Swahiyh kabisa. Kwa ajili hiyo natahadharisha kwa njia ya ujumla sisi sote kutoingilia magomvi haya ya kisiasa yaliyoko hivi sasa. Kwa sababu zama zenyewe ni za fitina. Kila ambavo zama zinakwenda mbele ndivo kutajitokeza upya mfano wa fitina hizi za kifikira.

[1] ”Kisiwa cha kiarabu kitakuja kuongozwa na bwana mmoja kwa ajina ”Hayawaan”… ”

Check Also

Hoja ya Hizbiyyuun kwa kisa cha Yuusuf ili kuingia bungeni

Miongoni mwa aina ya mfumo huu magazeti ya ndani yalichapisha (nafikiri ilikuwa ni Shaykh ´Umar …