Kutufu ambako ni Bid´ah na kufuru

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kulizunguka kaburi ikiwa haamini kuwa linanufaisha na linadhuru lakini hata hivyo anakusudia kujikurubisha kwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala)? Je, ahukumiwe ukafiri?

Jibu: Ni kama mfano wa mwenye kuswali kwa ajili yao. Ndio ni ukafiri. Ni kama mfano wa mwenye kuswali kwa ajili yao, akawaomba, akawataka uokozi, akaitakidi kuwa ni waombezi ambapo akawa anawaomba. Na si kwamba anaamini kuwa wanaumba, wanaruzuku au wanaendesha mambo. Anawaomba ili wamuombee. Hii ndio shirki kubwa. Ama akitukufu tu kwa kuona kuwa ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kama mfano wa Ka´bah, basi hii ni Bid´ah na ni njia inayopelekea katika shirki, jambo ambalo hutokea mara chache. Kutufu ambako hutokea mara nyingi mtu anakusudia kujikurubisha kwa yule aliyemo ndani ya kaburi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 50
  • Imechapishwa: 21/06/2019