Swali: Mwenye kuacha mambo ya kisasa; kama kupanda gari na kuishi kwenye manyumba ya kisasa anahesabika kuwa ni katika watu wenye kuipa nyongo dunia?
Jibu: Hapana. Huku ni kujikalifisha na kupetuka mipaka.
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ |
“Sema: “Nani aliyeharamisha mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea waja Wake na, vizuri katika riziki?” (07:32) |
Hakuna yeyote anayeharamisha Aliyohalalisha Allaah (´Azza wa Jalla) na kusema kuwa ni kuipa nyongo dunia. Lakini hata hivyo asifanye israfu. Awe kati na kati.
وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا |
“Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo.” (25:67) |
Asifanye israfu na wala asifanye ubakhili. Awe kati na kati. Haya ndiyo Aliyoweka Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Shari´ah. Haijuzu kuharamisha vitu vizuri Alivyoruhusu Allaah.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-4-23.mp3
- Imechapishwa: 09/11/2014