Kutokwa na mabaki ya maganda ya chakula kunaharibu wudhuu´?

Swali: Nilitawadha kwa ajili ya swalah na baada ya kutawadha kwa saa moja nikatokwa na chembechembe za maganda ya machungwa kwenye meno yangu. Sikuyajua hayo wakati nilipokuwa natawadha. Je, nirudi kutawadha upya?

Jibu: Hapana neno. Wudhuu´ wako ni sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 11/09/2018