Kutoitikia wito wa harusi wa muislamu

Swali: Je, mtu anapata dhambi ikiwa hakuitikia wito wa ndugu yake?

Jibu: Ndio. Karamu ya harusi ni wajibu, isipokuwa tu ikiwa kama kutakuwa kuna kikwazo:

“… na akikwita muitikie.”

Ni moja ya haki ya muislamu juu ya muislamu mwenzake. Akikwita muitikie. Walima wa harusi unatiliwa nguvu zaidi kuliko wito mwingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014