Kutochukulia jambo la kukusanya swalah ni la kimazowea

2837- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeyafanya haya ili Ummah wangu usije kupata uzito.”

Ameipokea at-Twabaraaniy (10525): Idriys bin ´Abdil-Kariym al-Haddaad ametuhadithia: Ahmad bin Haatim at-Twawiyl ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Abdil-Qudduus ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Tharwaan, kutoka kwa Zaadhaan ambaye amesimulia kuwa ´Abdullaah bin Mas´uud amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya kati ya Dhuhr na ´Aswr na Maghrib na ´Ishaa. Alipoulizwa sababu akasema: “Nimeyafanya haya ili Ummah wangu usije kupata uzito.”

Cheni ya wapokezi ni nzuri na wapokezi wake wote ni waaminifu, isipokuwa tu ´Abdullaah bin ´Abdil-Qudduus ambaye Ibn Hibbaan amemtaja katika “ath-Thiqaat”[1].

Kinachonibainikia ni kwamba kukusanya swalah katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas ni kwamba inafaa kukusanya swalah pale ambapo kuna ugumu. Vinginevyo haitojuzu. Uzito ni jambo linatofautiana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hali ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Pengine wale Salaf waliosema kuwa inafaa kukusanya swalah kwa njia ya kuachia wameshurutisha kile nilichokitaja kwamba mtu asichukulie jambo hilo kuwa ndio mazowea kama wanavofanya Shiy´ah. Jambo hilo siwezi kufikiria kuwa linaweza kufanywa na mtu ambaye anapupia kuswali vipindi vitano vya swalah ndani ya nyakati zake na misikitini pamoja na mkusanyiko – na Allaah ndiye anajua zaidi.

[1] ath-Thiqaat (7/48).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (6/2/817)
  • Imechapishwa: 10/08/2020