Swali: Baadhi ya watu wa mashambani wanatoa Zakaat-ul-Fitwr nyama. Je, inajuzu?

Jibu: Haya si sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Swaa´ ya chakula. Nyama inapimwa na wala haikadiriwi kwa kiasi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Swaa´ ya chakula. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr Swaa´ ya tende au Swaa´ ya ngano.”

Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Tulikuwa wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tukitoa Swaa´ ya chakula. Kipindi hicho chakula chetu kilikuwa ni tende, shayiri, zabibu na maziwa  ya unga[1].”

Kwa ajili hii maoni sahihi ya wanachuoni ni kwamba si sahihi kutoa Zakaat-ul-Fitwr katika pesa, nguo au magodoro. Maoni yanayosema kuwa ni sahihi kutoa Zakaat-ul-Fitwr pesa hayazingatiwi. Midhali kuna dalili ya wazi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayachukuliwi maneno ya yeyote. Busara haina haki yoyote ya kuonelea uchaguzi fulani katika kubatilisha Shari´ah. Hapana shaka ya kwamba Zakaat-ul-Fitwr si sahihi isipokuwa katika chakula. Chakula chochote cha nchi ni sahihi kukitoa kama Zakaat-ul-Fitwr.

[1] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Cottage_cheese

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/280-281)
  • Imechapishwa: 23/06/2017