Kutoa salamu pindi mtu anapotoka sehemu fulani

Swali: Kutoa salamu kabla ya kutoka msikitini baada ya kumaliza kuswali imethibiti? Tunawaona ndugu zetu wengi – Allaah awajaze kheri – wanatoa salamu kwa kusema: “as-Salaam ´alaykum” wanaposimama kwenye safu kwa ajili ya kutaka kutoka msikitini. Wanafanya hivo kwa ajili ya kupupia kwao kheri. Je, hili lina msingi? Linaingia katik Hadiyth zilizoenea ambazo zimepokelewa kuhusu mtu anaposimama kutoka kwenye kikao?

Jibu: Hili linaingia katika ujumla ya kwamba mtu anatakiwa kutoa salamu pindi anapoingia na kutoa salamu pindi anapotoka. Ama kusema kwamba kuna dalili maalum juu ya hili mimi sijui kama kuna dalili maalum juu ya hili. Lakini ule ujuma unatosheleza. Mtu anapotaka kusimama na kwenda zake atoe salamu. Kwa sababu anaenda zake. Isipokuwa ikiwa kama hilo linapelekea katika kushawishi wale wanaofanya Tasbiyh au wale wanaosoma. Katika hali hiyo usifanye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1070
  • Imechapishwa: 22/03/2019