Kutoa nafaka kwa maganda yake katika Zakaat-ul-Fitwr

Swali: Inajuzu kutoa Zakaat-ul-Fitwr kama vile mchele, mahindi, shayiri na mtama hata kama vitakuwa bado na maganda juu yake?

Jibu: Inajuzu kufanya hivo ikiwa ni miongoni mwa vyakula vinavyoliwa katika mji huo. Hayo ndio maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Lakini inatakiwa iwe baada ya kuvisafisha na maganda. Allaah (Subhaanah) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ

”Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma.”[1]

Kwa sababu huku ndio kutakasa dhimma na urafiki zaidi kwa yule fakiri. Isipokuwa tu shayiri si wajibu kuisafisha kutokamana na maganda kutokana na uzito unaopatikana wa kufanya hivo. Lakini pale atapotoa kutoka ardhini  shayiri na nafaka nyenginezo mfano wake ambazo manufaa zaidi ni kuziacha kubaki katika maganda yake muda wa kuwa atahakikisha ametekeleza wajibu wake kwa kile kiwango cha uadilifu, basi katika hali hiyo hakuna neno – akitaka Allaah – kwa ajili ya kuchunga manufaa ya bwana na fakiri.

[1] 02:267

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/206)
  • Imechapishwa: 12/06/2018