Kutoa mimba baada ya siku arubaini


Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa mimba kabla ya kutimiza siku arubaini kwa sababu ya mambo ya kinafsi na kijamii na khaswa pale ambapo mke anakhofia talaka huko mbeleni?

Jibu: Kutoa mimba haijuzu kwa sababu ya kutoridhia ujauzito. Lakini ikiwa madaktari watathibitisha kuwa kipomoko kinamtia mama khatarini na wanachuoni wakafutu kutokana na uthibitishaji huu, hapa ndipo mimba itaporomoshwa. Utoaji wa mimba sio jambo la mchezo. Sio kujitolea tu mimba. Madaktari wabobeaji ni lazima watoe uthibitisho. Baada ya hapo ni lazima kutolewe fatwa kutokana na uthibitishaji huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1434-08-14.mp3
  • Imechapishwa: 20/05/2018