Swali: Je, inajuzu kutoa kafara ya yamini mali?
Jibu: Hapana, hili halijuzu. Linaenda kinyume na andiko. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:
فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ |
”Basi kafara yake (ya kuvunja viapo hivi) ni kulisha maskini kumi…” (05:89) |
Amesema “Lisheni” na Hakusema “Toeni Swadaqah kwa masikini kumi”. Amesema “Lisheni” ambako maana yake ni kuwapa chakula masikini.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-6-9.mp3
- Imechapishwa: 15/11/2014