Kutengeneza keki na kadi katika minasaba ya sikukuu za kikafiri

Swali: Mfano wa siku kama hizi kila kunapoingia mwaka mpya wa kikafiri basi vitu tamtam kwa aina zake mbalimbali na keki zinakuwa nyingi na katika baadhi ya keki hizo kunaandikwa:

كل عام وأنتم بخير

“Uwe na mwaka mpya wenye furaha.”

Huenda vilevile wakachora mpaka msalaba. Je, inajuzu kwa wale wenye kutengeneza mikate hii kufanya mambo kama hayo na khaswa kwa kuzingatia ya kwamba wakati kama huu ndio wakati wenye soko kwao? Tunaomba ikiwa kama hukumu ni uharamu basi uwape nasaha watu hawa  na pia watu wenye kutengeneza vitabu kwa sababu hufanya vijikadi ambavyo vimeandikwa ibara kama hizi.

Jibu: Ninaapa ya kwamba kitu kama hichi ni haramu. Kitu kama hichi kinaweza kumfikisha mwenye nacho katika ukafiri. Kutoa pongezi kwa sikukuu za makafiri ina manaa ya kuridhia mambo na dini yao. Vilevile ni kuridhia ukafiri. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amegusia hilo katika kitabu “Ahkaam Ahl-id-Dhimmah” na kwamba haijuzu kuonyesha nembo yoyote ya kikafiri katika minasaba yake. Si halali kwa watu hawa wenye kutengeneza mikate wakafanya hivo; nako ni kule kuchora misalaba, mwaka mpya wenye furaha na mfano wa hayo. Allaah ametakasika kutokamana na kila upungufu na kasoro. Ni vipi tutawapongeza watu kwa sikukuu za makafiri ambao hawamuamini Allaah wala siku ya Mwisho? Isitoshe tunawapongeza watu kwa sikukuu za watu gani? Sikukuu za manaswara. Watu hawa wamezikeuka heshima za waislamu, wakahalalisha damu zao na wakaipora miji yao. Iwapo wangeliweza basi wangeliutokomeza Uislamu wote. Ni vipi tutawapongeza watu kwa sikukuu za watu kama hawa? Ninaapa kwa Allaah iwapo sikukuu ya kitaifa isingelikuwa ya Kishari´ah basi wasingelistahiki kupewa pongezi. Tusemeje ilihali kwa wao wanachukulia kwua ni sikukuu ya Kishari´ah na kwamba ni katika nembo za dini yao? Itambulike kuwa kuridhia nembo za kikafiri ni ukafiri. Hili ni jambo khatari kwenye mioyo. Kuna ukhatari moyo ukapinda na tunaomba ulinzi kutoka kwa Allaah. Hatimaye mtu anakuwa hawezi kutofautisha kati ya adui wa Allaah na mpenzi wa Allaah.

Sisi tunamshuhudisha Allaah kwa yale aliyosema: ya kwamba kila kafiri basi ni adui wa Allaah na kwamba kila kafiri ni adui wetu. Haya ni kwa dalili ya Qur-aan:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ

“Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa wapenzi na marafiki.”[1]

Ni vipi watu hawa ambao Allaah ameshuhudia kuwa ni maadui na sisi vilevile tunashuhudia kuwa ni maadui tutafuurahia sikukuu zao? Ni vipi tutazieneza kati ya watoto, wake wetu na wanawake wetu? Lakini si jengine isipokuwa huku ni kufa kwa mioyo, kuyeyuka kibinafsi na kuwafuata watu kichwa mchunga ndio jambo lililofanya mambo kama haya kuyaona ni mepesi kwetu.

Naonelea kuwa mambo haya ni haramu na kwamba ni wajibu kwetu kuzisusa sikukuu zinazofanywa kama alivyosema muulizaji. Vilevile ni wajibu kwa watengeneza mikate hawa wakome kuuza kadi hizi ambazo ndani yake kuna kuwapongeza kwa sikukuu za kikafiri ambazo hazimridhishi Allaah, Mtume wake wala waumini.

[1] 60:01

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (31) http://binothaimeen.net/content/698
  • Imechapishwa: 03/11/2017