Swali: Mtu ameingia msikitini siku ya ijumaa mapema na akatenga nafasi katika safu ya kwanza. Kisha akaenda sehemu ya nyuma msikitini na akalala kwa muda wa takriban saa mbili. Je, inafaa kufanya hivo?

Jibu: Hapana, haijuzu. Ametenga sehemu kwa ajili ya kulala? Haijuzu. Akitenga sehemu kwa ajili ya kwenda kutawadha au kukidhi haja yake kisha arudi, hakuna neno. Ama kusema kutenga sehemu kisha aende kulala. Kama unataka kulala nenda kulale na uache msikitini kwa wale walio macho na wanaokuja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahthat-12021440h.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2019