Kutenga mahali msikitini au kwenye darsa

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kujitengea mahali ambapo ni bora kwenye msikiti Mtakatifu au kwenye mizunguko ya kielimu?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kujitengea pahali. Ni lazima kwake kuja kwa nafsi yake. Kufanya hivi ni kupora. Isipokuwa akiwepo pale na pahali hapo ikawa ni mbele yake na akafanya hivo ili aweze kupumzika kidogo, kuegemea juu ya nguzo, ameenda kutawadha kisha arudi au akatangulia mwenyewe. Katika hali hizo hakuna neno. Ama kitendo cha kupenga pahali kisha akaenda zake. Halafu anakuja amechelewa kwa masaa marefu au anaenda kufanya biashara zake na huku kishaacha ametenga mahali. Matendo haya ni uporaji uliokatazwa na maudhi ya haramu. Sivyo tu, bali kufanya hivo kunaweza kupelekea katika chuki, bughudha na fitina. Kwa hivyo ni vizuri akaacha kwa ajili ya kuzuia madhara.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 29/06/2019