Kutembelea pango la Hiraa´, mlima wa Thawr na msikiti Qiblatayn

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzitembelea nafasi za historia ya kiutume kama pango la Hiraa´, mlima wa Thawr na msikiti Qiblatayn?

Jibu: Ikiwa matembezi yanahusiana na kufanya Tabarruk au yanatokamana na kuonelea kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah, ni Bid´ah. Haijuzu. Hata hivyo haina neno ikiwa mtu atayatembelea kwa ajili ya elimu. Ama ikiwa matembezi yanahusiana na kufanya Tabarruk au akawa anaamini kuwa kuyatembelea ni jambo limewekwa katika dini na lina ujira, hivyo itakuwa ni Bid´ah. Haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1434-08-14.mp3
  • Imechapishwa: 20/05/2018