Kutawadha kwa maji yaliyoandaliwa kwa ajili ya kunywa au kuoga tu

Swali: Ni ipi hukumu ya kutawadha kwa maji ambayo yameandaliwa kwa ajili ya kupata baridi?

Jibu: Wapo wanachuoni ambao wanaonelea kuwa wudhuu´ wake hausihi kwa sababu hayakuandaliwa kwa sababu ya kutawadha. Ni kama mfano mtu atawadhe kwa maji kutoka katika zile mashine za kufanya maji baridi kwa ajili ya watu kunywa ni sawa na kuswali katika ardhi iliyoibiwa.

Maoni ya pili yanasema kuwa wudhuu´unasihi pamoja na kwamba mtu anapata dhambi. Haya ndio maoni ya sawa. Anapata dhambi za kuiba na wakati huohuo anapata thawabu za swalah yake. Kwa sababu amekatazwa kuchukua maji kwa jengine zaidi ya kunywa.

Akiwa katika mji basi analazimika kutafuta maji hata kama swalah ya mkusanyiko itampita. Haisihi akafanya Tayammum katika mji ilihali anaweza kupata maji. Hakufanywi Tayammum isipokuwa wakati wa kukosekana maji au pindi hakuna uwezekano wa kuyatumia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2018