Kutania kwa kusema “Nimekuozesha msichana wangu”


Swali: Imethibiti katika Hadiyth Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mambo matatu ukweli ni ukweli na mzaha wake ni ukweli; [ndoa, talaka na kumrudia mkeo (baada ya kumtaliki)].”

Lau mtu atamwambia mwengine kwa kumtania “Nimekuozesha msichana wangu” na yule mwengine akaitikia “Nimekubali”.

Jibu: Mambo yamekwisha. Ameshakuwa ni mke wake. Hakuna mzaha. Ndoa haina mzaha. Ukweli ni ukweli. Hakuna mzaha kwa hilo. Talaka hakuna mzaha. Huwezi kuitoa kisha baadaye ukasema nilikuwa natania tu. Tunasema kuwa mke wako anaenda hata kama ulikuwa unatania. Mmiliki akiacha mtumwa huru na kusema amemuacha huru mtumwa wake, kisha baadaye akasema alikuwa anafanya mzaha tu. Tunasema hapana, mwache huru. Hakuna mzaha. Kadhalika akisema nimemrejea mke wangu na ikawa bado ni talaka rejea, inabidi arudi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13829
  • Imechapishwa: 20/09/2020