Swali: Mwenye kufanyia mzaha kitu katika dini ya Allaah anaamrishwa kutamka shahaadah upya kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwamrisha mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah atamke upya au inatosha kutubia tu?

Jibu: Akihukumiwa kuritadi basi ni lazima atamke shahaadah mbili. Akiwa alikanusha kitu katika mambo ya dini basi ni lazima kwako kukikiri alichokikanusha pamoja na kutamka shahaadah mbili. Ni lazima kutamka shahaadah mbili wakati wa kuingia katika Uislamu na wakati wa kutubu juu ya kuritadi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (06)
  • Imechapishwa: 29/12/2018