Kutamka nia ni Bid´ah


Nia mahala pake ni moyoni. Haina nafasi mdomoni katika matendo yote. Kwa ajili hii, yule mwenye kutamka nia wakati anapotaka kuswali, kufunga, kuhiji, kutawadh au matendo mengine yasiyokuwa hayo, anakuwa amezusha katika dini ya Allaah yasiyokuwemo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitawadha, akiswali, akitoa swadaqah, akifunga na akihiji bila ya kutamka nia. Alikuwa hasemi “Ee Allaah! Nanuia kutawadha”, “Ee Allaah! Nanuia kuswali”, “Ee Allaah! Nanuia kutoa swadaqah”, “Ee Allaah! Nanuia kufunga”, “Ee Allaah! Nanuia kuhiji” na kadhalika. Alikuwa hasemi hivi. Hilo ni kwa sababu nia mahala pake ni moyoni. Allaah (´Azza wa Jall) anajua yaliyomo ndani ya moyo na hafichikani na chochote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/13)
  • Imechapishwa: 26/12/2017