Kutakharuji kwenye chuo kikuu cha Kiislamu – ufunguo wa kuanza kutafuta elimu

Swali: Mwenye kutakharuji kwenye chuo kikuu cha Kiislamu chenye kitivo cha Shari´ah anakuwa ni mwenye kustahiki kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah na kubainisha mfumo wa haki?

Jibu: Wenye kutakharuji kwenye chuo kikuu cha kitivo Shari´ah wanatofautiana. Baadhi yao wanatoka wamepata elimu yenye manufaa. Wengine wanatoka wamepata shahada ya karatasi na hawajui walichokisoma kwa sababu wamesoma na kumaliza. Hawalingani. Allaah Humtunukia yule Amtakaye katika waja Wake. Wanatofautiana. Hata hivyo tunawadhania vizuri na kuwaambia wasitosheke na kusoma kwenye kitivo cha Shari´ah. Ni ufunguo tu. Ni ufunguo tu na mlango wa elimu. Endeleeni kusoma.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu’
  • Imechapishwa: 05/09/2020