1Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 2Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 3Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 4Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 5Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mwanzo 21:01
  • Imechapishwa: 14/01/2020