Kutahiriwa kwa Abrahamu na Ismaeli


23Siku ileile Abrahamu akamchukua mwanawe Ismaeli na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. 24Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 99 alipotahiriwa, 25naye Ismaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka 13. 26Abrahamu na Ismaeli mwanawe walitahiriwa siku ileile, 27Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mwanzo 17:23
  • Imechapishwa: 13/01/2020