Swali: Je, kumtahadharisha mtu wa Bid´ah, mwenye kufuata matamanio yake na mapote ya uzushi ili waislamu wa kawaida wasidanganyike ni katika usengenyi uliosemwa vibaya?

Jibu: Kutahadharisha wapotevu ni wajibu. Kutahadharisha kosa la kidini ni jambo la wajibu na ni kuwapendea kheri waislamu. Sio kusengenya. Kwa kuwa mtu anakusudia kunasihi na kumtukana yule mtu. Itakuwa ni kusengenya ikiwa lengo ni kumtukana mtu. Ama ikiwa makusudio ni kuwatakia waislamu kheri na kuwawekea watu kosa wazi ni nasaha. Dini ni  kupeana nasaha, hivyo ndivyo alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 12/11/2017