Swali: Je, nimtahadharisha mlinganizi katika nchi yangu ambaye ana kosa la ´Aqiydah baada ya kuthibiti kosa hili au nisubiri kwanza mpaka waseme wanachuoni wakubwa katika nchi yangu?
Jibu: Ikiwa una uhakika kwamba kweli ana kosa, basi wewe unatakiwa kuwabainishia kwanza huenda akajirudi. Ikiwa ataendelea kung´ang´ania na asijirudi, basi wabainishie watu yale makosa alionayo.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (79) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-9-2-1439-01.mp3
- Imechapishwa: 09/03/2018