Kutafuta riziki au elimu?


Swali: Mimi ni mwanafunzi. Familia yangu hali yao ya kiuchumi si nzuri. Je, kutafuta kwangu riziki, kuwahudumia na kuwasaidia ndio bora kuliko kutafuta kwangu elimu na kuhudhuria darsa?

Jibu: Ndio. Ikiwa hali ni kama hii basi kutafuta kwako riziki itayokufaa wewe na wao ni bora kuliko kuhudhuria kwako darsa. Lakini kuna uwezekano ukakusanya kati ya hayo mawili kwa njia ya kwamba ukafanya kazi na unapofika wakati wa darsa ukaenda kuhudhuria darsa kisha ukarudi kazini. Kwa njia hiyo ukawa umekusanya kati ya yote mawili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (49) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/m-3%20%20-%2012%20-%202%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2018