Kutafuta elimu kwa kuwapigia simu


Swali: Je, inajuzu kutafuta elimu kwa njia ya kuwasiliana na wanachuoni Rabbaaniyyuun[1] kwa simu au ni lazima nikae pamoja nao katika durusi na mihadhara?

Jibu: Kuwapigia simu kwa ajili ya kuwauliza maswali ni sawa. Ama kuwapigia simu kwa ajili ya kujifunza hapana. Hili si sawa na haifai. Ni lazima uende kwa wanachuoni, kukaa pamoja nao, kusikiliza durusi zao na kuwauliza maswali ana kwa ana. Huku ndio kutafuta elimu.

[1] Tazama http://wanachuoni.com/content/maana-ya-wanachuoni-rabbaaniyyuun

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14005
  • Imechapishwa: 16/04/2018