Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kutafakari na kuzingatia hali za siku ya Qiyaamah; kama kupasukapasuka kwa mbingu, kuteremka kwa Malaika na watu kutoka ndani ya makaburi yao?

Jibu: Mtu anatakiwa kuzingatia na kukumbuka hali za siku ya Qiyaamah. Lengo ni iwe kichocheo, moyo wake uweze kutikisika na iwe sababu ya kumfanya awe na unyenyekevu. Jengine hayo yamfanye kumtakasia matendo yake Allaah (´Azza wa Jall), kutekeleza haki mbalimbali na kujiepusha na mambo ya haramu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 30/09/2018