Kutaabiri Kwa al-Albaaniy Kuhusu Mustaqbal Wa Salmaan al-´Awdah


Masikitiko makubwa ajali – uasi Algeri – ikatokea. Mpaka hivi leo ndugu zetu wanawasiliana na sisi. Ninaonelea kuwa kuna upumbavu na ujinga katika wao na natumai hamtochukulia vibaya. Kuna upumbavu na ujinga. Wananiuliza:

“Tufanye nini?”

Najibu:

“Kwani mnaweza kufanya nini? Sijui. Mnaweza kufanya nini?”

Wanajibu:

“Hakuna.”

Na mimi nasema “hakuna.” Hili ndio jibu.

Haya yana mafungamano na yale ambayo ndugu yetu Rabiy´ [al-Madkhaliy] aliyotaja kuhusu [Salmaan] al-´awdah, au wengine, na kwamba wanajishughulisha na siasa. Mimi naonelea kuwa mwisho itakuja kuwafanya kupita katika mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun, wa kialgeria na wa kambi ya Kiislamu.

Hili ndio jibu langu. Elimu juu ya Qur-aan na Sunnah ndio ambayo inazalisha wanaume ambao wanauokoa Ummah katika hali mbaya waliyomtumkia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (511)
  • Imechapishwa: 23/04/2015