Swali: Mtu akipitwa na Witr anaweza kuiswali baada ya adhaana ya fajr?

Jibu: Alfajiri inapoingia hakuna Witr. Anaweza kuikidhi baada ya jua kuchomoza pamoja na ile shafa yake; ikiwa amezowea kuswali Rakaa´ tatu aswali nne kwa Tasliym mbili, ikiwa amezowea kuswali tano aswali sita na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (8) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340429.mp3
  • Imechapishwa: 10/02/2017