Swali: Niko katika kitengo cha kijeshi. Wakati wa Dhuhr baadhi ya wafanya kazi wanaswali warsha pamoja na kuwa msikiti uko karibu. Hoja yao ni kwamba nguo zao zina uchafu wa mafuta na mengineyo ndio maana hawataki kuchafua msikiti. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa wayasemayo ni sahihi na wana harufu mbaya na nguo zao zina uchafu, wasiendi msikitini. Waswali mkusanyiko hapo walipo. Ni wenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 24/05/2018