Kuswali Tarawiyh msikitini ni bora kuliko nyumbani


Swali: Je, nende msikitini au niswali nyumbani kwangu? Mimi sio imamu bali ni maamuma na napenda kusoma Qur-aan. Nafadhilisha kusoma mwenyewe kuliko kumsikiliza mwengine akisoma. Nina dhambi iwapo nitaswali Tarawiyh tu nyumbani?

Jibu: Hakuna dhambi kwako kuswali nyumbani kwa sababu ni sunnah. Lakini hata hivyo kuswali msikitini pamoja na imamu ndio bora zaidi kwa kumuiga Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Wakati Mtume aliwaswalisha Tarawiyh kama takriban nyusiku tatu ambapo baadhi yao wakamwambia: “Si utuswalishe sehemu ya usiku iliobaki?” Akasema:

“Mwenye kusimama pamoja na imamu mpaka akamaliza basi ataandikiwa kama amesimama usiku mzima.”

Ameipokea Ahmad na waandishi wa “as-Sunan” kwa cheni ya wapokezi nzuri kupitia kwa Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=36&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 21/05/2018