Kuswali Tarawiyh kabla ya kutangazwa kwa mwezi mwandamo

Swali: Baadhi ya maimamu huanza kuswali Tarawiyh kabla ya kutangazwa kuandama kwa mwezi. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Ni jambo lisilotakikana. Tarawiyh imesuniwa katika Ramadhaan. Haitakikani kwa yeyote kuiswali mpaka mahakama itangaze kuonekana kwa mwezi mwandamo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/26)
  • Imechapishwa: 08/05/2020