Kuswali swalah za faradhi mbili kwa wudhuu´ mmoja

Swali: Inajuzu kwa mtu kuswali swalah za faradhi mbili kwa wudhuu´ mmoja?

Jibu: Ndio, inajuzu kufanya hivo. Kwa mfano akitawadha kwa ajili ya swalah ya Dhuhr kisha kukafika swalah ya ´Aswr ilihali bado yuko na twahara, inafaa kwake kuswali swalah ya ´Aswr kwa wudhuu´ wa Dhuhr. Hata kama wakati wa kutawadha hakunuia inafaa kwake kuswali kwao faradhi mbili.  Kwa kuwa wudhuu´ aliyotawadha kwa ajili ya kuswali Dhuhr umeondosha hadathi. Hadathi ikiondoka basi hairudi isipokuwa kwa kupatikana sababu yake ambayo ni kuwemo moja katika vile vitenguzi vya wudhuu´ vinavyotambulika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/150)
  • Imechapishwa: 01/07/2017