Kuswali swalah ya mkusanyiko hospitali


Swali: Hospitali kunaswaliwa swalah nyingi za mkusanyiko ilihali misikiti iko karibu. Je, ni lazima  kwenda msikitini kutokana na kwamba iko karibu au tutosheke na swalah hizi za mikusanyiko ndani ya hospitali?

Jibu: Hili linahitajia upambanuzi. Yule ambaye analazimika kuweko hospitali, kama mfano wa mlinzi, mgonjwa asiyeweza kufika msikitini na mfano wake, basi haimlazimu kutoka kwenda msikitini. Bali ataswali mahala pake pamoja na mkusanyiko ambao anaweza kuswali nao. Kuhusu ambaye anaweza kufika msikitini basi atalazimika kwake kufanya hivo kwa ajili ya kutendea kazi dalili za Kishari´ah. Miongoni mwazo ni maneno yake  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yeyote atakayesikia wito [wa adhaana] na asiuitikie, basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.” Akaulizwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): ”Udhuru ni nini?” Akajibu: ”Khofu au maradhi.”

Ameipokea Ibn Maajah na ad-Daaraqutwniy  na ameisahihisha Ibn Hibbaan na al-Haakim na cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/29)
  • Imechapishwa: 05/02/2021