Swali: Ambaye amepitwa na Swalah ya al-Fajr pasina khiyari yake na ni katika watu wenye kuhifadhi Swalah ya Jamaa´ah na hakuamka isipokuwa wakati kunapokimiwa kwa ajili ya Swalah ya Ijumaa, kisha akaswali Ijumaa kwa nia ya al-Fajr na baada ya hapo akalipa Dhuhr Rakaa nne. Je, kitendo chake hichi ni sahihi?

Jibu: Hapana, sio sahihi. Alitakiwa kuswali al-Fajr kwanza Rakaa mbili kisha ndio akaswali Ijumaa. Angeanza kuswali al-Fajr kisha ndio akaswali Ijumaa hata kama Ijumaa atawahi Rakaa ile ya mwisho tu. Anatakiwa kuswali al-Fajr kwanza Rakaa mbili kisha aingie pamoja na imamu kwa zile Rakaa zitazokuwa zimebaki za Ijumaa. Ikiwa amewahi Rakaa moja kikamilifu, aitimize kwa sura ya Ijumaa. Ikiwa hakuiwahi [Rakaa moja] kikamilifu, aitimize kwa sura ya Dhuhr.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_06.mp3
  • Imechapishwa: 29/06/2018