Kuswali pasina kusujudu


Swali: Kuna mwanamke ilimhudhuria yeye Maghrib kipindi ambapo alikuwa mbele ya wanamme mahali pa umma. Hakuweza kujificha nao wakati wa swalah yake. Lakini aliogopa wasije kumfitinisha. Je, ana haki ya kuswali pasi na kusujudu?

Jibu: Hana haki ya kufanya hivo. Lakini atafute maeneo mengine ijapo atachelewesha swalah kwa muda wa saa moja au nusu saa. Wakati ni mrefu ikiwa ni Dhuhr au ´Ishaa. Asubiri mpaka pale Allaah atapomfanyia wepesi wa kupata mahali pa mbali na wanamme ili anyenyekee katika swalah yake. Ajaribu kuwa nyuma ya gari au kitu kingine. Kuhusu kuswali pasi na kusujudu  swalah hiyo haisihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 14/08/2021