Swali: Inajuzu kuswali nyuma ya imamu ambaye anajulikana kuwa ni Suufiy?

Jibu: Ikiwa Bid´ah zake hazimtoi katika Uislamu swali nyuma yake. Lakini hata hivyo inatakiwa kubadilisha mwengine ikiwa inawezekana. Usiache swalah ya mkusanyiko.

Ikiwa Suufiyyah yake inamtoa katika Uislamu, kama kumuomba mwengine asiyekuwa Allaah au kuchinja kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah, usiswali nyuma yake. Ni mamoja kawa ni Suufiy au asiyekuwa Suufiy. Haijuzu kuswali nyuma yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (34) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid-17-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017