Kuswali nyuma ya mswaliji baada ya kuchelewa

Swali 12: Kundi la watu likiingia msikitini na wakakuta kwamba wameshapitwa na swalah ya mkusanyiko na wakamkuta mtu anaswali peke yake. Je, inafaa kwao kuswali nyuma yake?

Jibu: Dhahiri ni kwamba wanatakiwa kuswali kivyao. Waswalishwe na yule ambaye ni msomi zaidi yao. Kwa sababu yeye ndiye ana kingi zaidi yao. Yule mwingine ana khiyari; akitaka ataikata swalah yake na kuswali pamoja nao na akitaka ataikamilisha swalah yake. Inatosha mtu mmoja akampa swadaqah kwa kuswali pamoja naye. Lakini akiikamilisha swalah yake peke yake hakuna neno na swalah yao inasihi japokuwa atakuwa hakunuia uimamu. Alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi mtu alipoingia na akawa ameshapitwa na swalah ya mkusanyko:

“Ni nani atakayempa swadaqah huyu na akaswali pamoa naye?”[1]

[1] Abu Daawuud (574), Ahmad (11613), al-Haakim (1/209), Ibn Hibbaan (2398) na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam as-Swaghiyr” (606) na (665). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”at-Ta´liyqaat al-Hisaan ´alaa Swahiyh Ibn Hibbaan” (7/574).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 28/09/2018